|
Asasi
ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na
mbegu zake imeadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa
kijiji cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Maadhimisho
hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili
kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya
‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo
biashara.
Afisa
ufundi wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima
kuhusu mbinu bora za uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu
katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji
cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
Katibu
tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi,
akisiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA
Bw. Giliard Daniel
katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji
cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...