TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa kongamano la watafiti na wanasayansi wa sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11 hadi 16 Novemba mwaka huu.

Kongamano hilo linatajiwa kuhudhuriwa na washiriki 550 ambapo kati yao Watanzaniani 250 na wageni kutoka nje ya nchi wanatarajia kuwa 300. Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jumanne (Septemba 16, 2014), Jijini Dar esSaalaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mgoo alisema lengo la kongamano hilo ni kuimarisha sekta ndogo ya ufugaji nyuki kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa katika kongamano hilo wadau hao pia watajadili kwa pamoja namna bora zaidi ya kusaidia mchango wa sekta hiyo katika Nyanja zautafiti, teknolojia pamoja na kubadilishana uzoefu katika uboreshaji, utunzaji na usimamizi wa makundi ya nyuki kwa uzalishaji wenye wingi na ubora.

“Kongamano litahusisha uwasilishwaji wa mada za utafiti kwa njia za mijadala, semina kwa wafugaji nyuki, majadiliano ya kitaalamu sanjari na maonyesho ya bidhaa za ufugaji nyuki” alisemaMgoo.

Aidha Mgoo alisema washiriki wote watapaswa kujilipia ada ya ushiriki ikiwemo gharama za usafiri na malazi, ambapo kwa kutambua ukubwa wa gharamahizo Serikali ililazimika kulipia baadhi ya huduma. “Gharama za mtu mmoja kwa siku ni dola za kimarekani 120 ila mshiriki wa Tanzania hulipaTsh. 150,000/- tu” alisema Mgoo.

Kwa mujibu wa Mgoo mbali na kongamano hilo, washiriki hao pia watapata fursa ya kushiriki ziara ya mafunzo, kwa kutembelea maeneo mbalimbali yanayojihusisha na ufugaji nyuki nchini ikiwemo Mkoawa Kilimanjaro, ambapo wataweza kujionea ufugaji nyuki wasiouma pamoja na ufugaji nyuki katika nyanda kame za Mikoa ya Singida na Dodoma.

Kwa wake upande Rais wa Shirikisho la UfugajiNyuki Duniani (Apimondia) Gilles Ratia amesifu maandalizi mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha na kuwezesha mkutano huo nchini.

Akizungumzia sekta ya ufugaji nyuki nchini, Ratia amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali katika kuwasaidia na kuwaendeleza wafugaji wa nyuki, na hivyo kuwataka wafugaji kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo litakaloweza kuwajengea uwezo katika uzalishaji na hivyo kuwaongozea kipato.
“Napenda kutoa pongezi zangu kwaMhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaj itihada zake anazozionyesha katika kusaidia na kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki kwani ameonyesha nia ya dhati ya kusaidia sekta hii” alisema.
Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne (Septemba 16, 2014) kuhusu kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto ni Afisa Nyuki Mwanadamizi, Stephen Msemo, kulia ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...