Warembo
15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014
wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam,
Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la
kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara.
Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya
shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya
wengine 15 kufanyika Arusha mjini.
Msanii wa Bongo Fleva Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
Tanzania si mchezo kwa vimwana!
ReplyDeleteDu Watoto wakaliii !
Hivi ninyi wasichana mpo kweli huko shamba Babati?
Mnhhh ama kweli tukimbilie wapi?
ReplyDeleteHuku Mijini wapo wapaka Lipstick kwenye kope za macho, na huko Babati wasichana ni wakali kama hivyo, ahhh jamani tukimbilie wapi ili tuweze kuchanga?, hivi tutaweza kujenga majumba kweli?
Ahaaa!
ReplyDeleteBabati ndio kwa kwenda kutafuta wachumba wa kuoa!