Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe "Lilinga" ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. 
Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. 
Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. 
Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Kwa habari hii na zingine kibao ungana na mkongwe John Kitime katika libeneke lake jipya....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hapo mumechapia maana ya neno Iringa lilitokana na neno la kihehe linasema kwiringa maana yake ni mawe yanayorushwa kutoka mlimani- yaani wakati huo wajerumani walikuwa wakirusha mabomu pale kalenga kutoka mlimani sasa wao wakajua kwamba ni mawe. Uko hapo mwenyekiti. Nenda pale alikozikwa chifu Adam Sapi utapewa hadithi nzima

    ReplyDelete
  2. Historia nzuri! Kwa nini waheh hamjadai fidia kutoka kwa Wajerumani kuvamia ardhi yenu?!

    ReplyDelete
  3. Nice articles, hasa hizo za bendi za zamani. Kuna picha na habari za Idd Nhende, jee kuna mtu aweza kutupa habari zaidi za jamaa huyu?

    ReplyDelete
  4. Kama ni kudai fidia kutoka kwa wageni kuvamia nchi, basi si Wahehe tu. Ni Tanzania nzima au labda Afrika yote! Tafsiri ya Iringa kutokana na jina Lilinga ni sawa kabisa, wala si kutupa mawe! kumbuka pia sisi Wahehe hatuna "R", tuna "L" tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...