Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Imeanza rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu Mkoa wa Morogoro pamoja na uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki kwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero ambao zoezi la Ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho lilishafanyika. Kuanza kwa usajili na Utambuzi wa Watu mkoa wa Morogoro kumefuatia kukamilika kwa zoezi kama hili mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara ambapo sambamba na usajili unaoendelea sasa mkoani Morogoro zoezi la uchukuaji alama za vidole picha na saini ya kielektroniki limekuwa likiendelea katika baadhi ya Wilaya za mkoa wa Pwani.

Mkoani Morogoro; katika eneo la Mikese kijiji cha Fulwe tumeshuhudia msururu wa watu wakisubiri kusajiliwa huku wengine wakiwa katika harakati za kuingizwa katika Rejesta ya Makazi inayomilikiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Vijiji. Kwa utaratibu wa sasa ili uweze kusajiliwa lazima kwanza kuwa unatambulika katika serikali yako ya Mtaa/Kijiji na kuwa umeorodheshwa katika Rejesta ya Makazi ya Mtaa au Kijiji husika.
Leo ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi hilo litakalodumu kwa siku saba mpaka Jumapili ya tarehe 29/09/2014 wananchi wengi wameonekana kuhamasika na kujitokeza kwa wingi katika siku ya kwanza tofauti na mazoea ya wengi kujitokeza siku za mwisho za zoezi.

Changamoto kubwa bado imebaki wananchi wengi kukosa Viambata msingi vya kuwatambulisha kama vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu ya msingi au sekondari n.k jambo ambalo limekuwa likisisitiziwa sana na NIDA katika kurahisisha utambulisho wa mwombaji. (Picha na Rose Mdami- NIDA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ILI MTU AKUBALIKE KUPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA LA TANZANIA ANATAKIWA AONYESHE VITU GANI WAJUE KUWA NI RAIA HALALI WA TANZANIA, MAANA NAMNA NYINGINE MNAWEZA KUGAWA VITAMBULISHO NA KWA WAGENI PIA.

    ReplyDelete
  2. WAKENYA WAPO WENGI SAN HAPA TZ HASA UKIANGALIA MIKOA ARUSHA KILIMANJARO SO ITABIDI SERIKALI IWE MAKINI SAN KWAN HAWA JAMAA WATATUMIA MBINU ZOTE NAO WAPATE KITAMBULISHO CHA TAIFA KITU AMBACHO KITAKUWA C SAHIHI MBINU MBADALA INAHITAJIKA KWA KUGAWA VITAMBULISHO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...