Balozi wa Marekani Nchini Tanzania,
Mark Childress
Siku ya Kimataifa ya Utalii ambayo huadhimishwa tarehe 27 Septemba inatupa fursa ya kutafakari manufaa na matokeo ya jitihada za uhifadhi wa wanyama pori na utalii kwa jamii zinazozunguka maeneo ambapo shughuli hizi zinafanyika na kwa Tanzania kwa ujumla. Kwa watu wengi duniani kote, kutembelea Tanzania ni jambo la kipekee na la kihistoria katika maisha yao. Kwa Tanzania ziara za watalii hao ni chanzo cha mapato na kichocheo cha uchumi, ambacho kwa makadirio ya mwaka 2013 kililiingizia taifa takriban Dola za Kimarekani Bilioni 1.9. Wengi wa watalii hawa hutembelea Tanzania ili kujionea wanyama pori. Hata hivyo kwa bahati mbaya jambo hili hivi sasa linakabiliwa na kitisho.

Ujangili na utoroshwaji wa wanyama pori unatishia kuendelea kuwepo kwa mali asili hii adhimu na ya kipekee na mchango wake kwa uchumi. Ninapongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kukabiliana na kitisho hiki. Mimi mwenyewe binafsi nimedhamiria kwa dhati kabisa kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na ujangili na utoroshwaji wa wanyama pori.

Serikali ya Marekani itaendelea na ushirikiano wake wa muda mrefu na Tanzania katika eneo hili na imepanga kutoa zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 40 katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili kusaidia shughuli mbalimbali za uhifadhi na usimamizi wa wanyama pori. tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wanajamii katika maeneo husika, sekta binafsi na hata wafadhili wengine katika kusaidia jitihada hizi   zinazoongozwa na Watanzania wenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Juhudi za kulinda maliasili ikiwamo tembo na faru ziendelee ili viumbe hivi viendelee kuwa vivution vya utalii, na kuwepo vizazi vijavyo. Tunashukuru kwa misaada itumike kuhifadhi maliasili na kupambana na ujangili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...