Madereva hapa nchini wametakiwa kufuata sheria ya matumizi bora ya barabara ili kuepusha madhara yanayosababisha kupoteza maisha ya watu,ulemavu wa kudumu na upotevu wa mali.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani inayofanyika kitaifa mkoani Arusha,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uagizaji wa magari nchini ya Be Forward Tanzania,Daniel Mtaalam amesema njia hiyo ndio suluhu za ajali zinazotokea mara kwa mara.
Amesema wao kama wadau wa barabara wamekua miongoni wa wadhamini wakuu wa Wiki ya usalama barabarani katika kuhakikisha sheria za zinazingatiwa ili kuepusha hasara zinazojitokeza pindi ajali zinapotokea.Wadhamini wengine ni kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom na kampuni ya mafuta ya Puma.
“Iwapo madereva watazingatia matumizi sahihi ya sheria za barabarani ,naamini ajali zitapungua kwa asilimia kubwa jambo ambalo litakuza uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.”alisema Daniel
Kampuni ya Be Forward Tanzania ni waagizaji wakubwa wa magari kutoka nchini Japan wakitoa huduma katika nchi mbalimbali kusini mwa jangwa la Sahara huku wakiwa wametoa ajira kwa watu zaidi ya 250 wanaofanya kazi katika idara mbalimbali.
Amebainisha kuwa mchango wa kiuchumi unaotokana na kampuni hiyo hapa nchini ni mkubwa kwani kila mwezi wastani wa magari elfu kumi huagizwa kupitia bandari ya Dar es Salaam hatua inayoongeza mapato ya nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake, Afisa Ubora wa kampuni hiyo,Lazaro Elias alisema kutokana na kuwa ni wadau wa usalama barabarani wataendelea kuiunga mkono serikali katika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara ili kuokoa maisha ya watu.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(kulia)akimkabidhi Ngao Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uagizaji wa magari ya Be Forward Tanzania Co.LTD,Daniel Mtaalam ya kuwa Mdhamini Mkuu wa Wiki ya Usalama barabarani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...