Spika wa Bunge la Jumuiya ya
AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa
mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya
AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa
kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya
Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
: Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni
katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya
ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara
ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki
akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha
Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka
kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya
Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.
Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za
uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya
kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo
wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere
(katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki
katika Taasisi hiyo. Kitengo Cha
Mawasiliano Serikalini
Wizara ya
Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...