Mwanahabari Vedasto Msungu wa ITV (kushoto) na David Rwenyagira (Radio 5) walikuwa miongoni mwa wanahabari waliofika nje ya Jengo la Mahakama Kuu ya Pretoria ambapo ilikuwa siku muhimu ya utoaji hukumu kwa mwanariadha Oscar Pistorius aliyeshitakiwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake kwa silaha. Unayoyaona hapo nyuma ni magari maalum ya urushaji tukio hilo moja kwa moja katika vyombo mbalimbali vya habari duniani(OB Van) na mahema meupe ni Kambi iliyopigwa na wanahabari hao kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo muhimu.
Wanahabari Vedasto Msungu na David Rwenyagira walipata nafasi ya kumhoji raia huyu wa Afrika Kusini juu ya maoni yake kwa hukumu iliyotarajiwa kutolewa.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 waliweza kufika hadi katika Hifadhi ya Taifa ya Pilanesberg ili kujionea wanyama mbalimbali. Kutoka Kushoto ni Mtanzania Peter Masika anayeishi Johannesburg, Vedasto Msungu (ITV), Pascal Shelutete(Meneja Mawasiliano TANAPA) na Gerald Kitabu wa The Guardian.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...