Taasisi
isiyo ya kiserikali ya MAYEPS Tanzania imezindua kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE
FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri
au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati
wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu.
Akizungumza
na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam, Meneja wa Taasisi
hiyo John Masumba amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wafanyakazi katika jamii ya
Kitanzania hawaweki akiba kwa ajili ya kuwekeza kwa madhumuni ya kujenga uchumi.
Meneja
Masumba amesisitiza kuwa MAYEPS imetambua kwamba ikiandaa warsha moja kwa mwezi
juu wafanyakazi kufanya maamuzi yaliyo sahihi, itawafikia watu 600 kwa mwaka.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya aliwapitisha waandishi wa
habari juu ya yaliyomo kwenye kitabu hicho kwa kuendesha warsha fupi iliyowafungua
macho waandishi hao kuhusu namna ya kutunza fedha kuandaa maisha ya baadaye.
Akinukuu
kauli ya mtaalamu wa uongozi John Maxwell Mwenyekiti huyo alisema kuwa “Watu wanaofanikiwa
na wasiofanikiwa hawatofautiani sana kiuwezo bali wanatofautiana katika dhamira
ya kufika kilele au upeo wa uwezo wao”.
Mang’enya
aliongeza kuwa jukumu la kujenga maisha binafsi lipo kwa muhusika binafsi, hivyo, watumishi
wawe na msimamo sahihi utakaowawezesha kuwa na maisha bora.
Aidha,
MAYEPS hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa
Umama na binafsi namna ya kupanga matumizi. Pia hutoa
mafunzo ambayo yatawezesha wafanyakazi
kutambua kuwa fedha za mafao au pensheni hupungua thamani mwaka hadi mwaka hivyo
uwekezaji wa fedha hizo ni muhimu ufanywe kwa uangalifu.
Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya na kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba.
1 Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Rose Mang’enya wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI” hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba na Afisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Eleuteri mangi (kulia). (Picha na MAELEZO).
Mayeps Hongereni sana!
ReplyDeleteWatanzania tumedumaa sana ktk suala la kuweka akiba, watu wakiishi maisha ya ponda mali kufa kwaja wakati huohuo (endapo je kama ukiwa umefikia uzeeni hujakufa je itakuwaje?) kwani tukumbuke ya kuwa pia vilevile Fainali Uzeeni!