Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Michael Nagu akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha kutengeza mitambo  ya kutumika kwenye viwanda  vidogo vya bia, maziwa ya kawaida na maziwa ya soya. Mitambo hii ni kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa nia ya kuwezesha watu kiuchumi, kutoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani mazao ya kilimo. Serikali ya Ubelgiji inagharamia asilimia hamsini ya ununuzi wa mitambo hiyo. Mhe Nagu ametembelea kiwanda hicho leo Ghent Ubelgiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ingeleta tija zaidi kama waziri angeongozona na baadhi ya wafanyabiashara wa chini na kati iliwaeze kujifunza kile wenzetu wanafanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...