Waziri wa Viwanda na
Biashara Dr. Abdallah Kigoda akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya wiki ya
huduma za kifedha na uwekezaji yaliyoshirikisha zaidi ya wajasiliamali 3500
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Viwanda na
Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa Exim Bank
Agnes Kaganda baada ya benki hiyo kushinda nafasi ya tatu kwenye mafunzo ya
wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na
Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa Benki ya Watu
wa Zanzibar (PBZ) Badru Idd baada ya benki hiyo kushinda nafasi ya pili kwenye
mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na
Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa CRDB Albert
Michael baada ya benki hiyo kushika nafasi ya kwanza kwenye mafunzo ya wiki ya
huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
======== ======= =======
Dar es Salaam. Mafunzo na Kampeni
za uhamasishaji nchini Tanzania zitachangia katika kuongeza kasi ya kufanikisha
azma ya kutekeleza mpango wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa
Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda wakati akifunga Mafunzo ya Wiki ya
Huduma za Kifedha na Uwekezaji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Semina hiyo iliyoshirikisha wajasiliamali 3,500
kutoka sehemu mbali mbali nchini iliratibiwa na Kampuni ya NUEBRAND na
kufadhiliwa na wizara ya viwanda na biashara, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,
taasisi ya PESCODE, Tanzania Standard Newspapers, Sayona, Times FM na Kampuni
ya Ulinzi ya Kiwango.
Alisema shughuli hizo zinasaidia kusogeza huduma
karibu na jamii ya Watanzania ambao wote kwa viwango balimbali ni wawekezaji.
“Wengi wanafikiri wawekezaji ni wakubwa tu.Hapana.
Wakulima, wajasiriamali hata wamachinga pia,” alisema Waziri Kigoda.
Alisema kuwa muhimu ni kuwa na uongozi unaoratibu
shughuli hizo na kuzingatia nidhamu ya kujua uongozi uliopo.“Hali hii
itapunguza matatizo mengi yanayoendelea sasa kwa wamachinga,” alisema Waziri
Kigoda.
Aidha, Dk Kigoda aliongeza akisema
wafanyabiashara wote, kwa viwango vyao tofauti wanategemeana kuanzia wamachinga
mpaka ngazi ya mitaji mikubwa. Alisema ili kufikia hali hiyo, wawekezaji wa
makongamano, mafunzo na kampeni husika ipo haja ya kuendelea kutumia mitandao
na mifumo ya teknolojia mbalimbali katika kuelemisha namna ya kufikisha huduma
za kifedha kwa wawekezaji wanaoshiriki katika minyororo ya kuongeza thamani.
“Katika thamani hizo kuna bidhaa za kilimo,
ufugaji, madini, misitu, uvuvi hasa vijijini na hata sekta ya huduma
inayojumuisha utii, afya na elimu,” alisema na kuongeza: “Niwaambieni na kuwafahamisha kuwa moja ya malengo
ya Sayansi ni kubuni na kuunda teknolojia na utaratibu wa kufanya kazi zenu ili
kutumia mali ghafi na nguvu kidogo, kupata vingi kutoka vichache, kwa manufaa
ya taifa.”
Ili kuhakikisha tekinolojia inaleta ufanisi, Waziri
Kigoda alisema, ni muhimu sana kujikita katika matumizi bora na fursa
zinazojitokeza kupitia teknmolojia. “Wito wangu ni kwa taasisi za fedha, na zile za
utafiti na sayansi kuendelea kushirikiana na serikali kuona ni jinsi gani
tutaendeleza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kupata huduma za kifedha
kwa watu wengi zaidi,” alisema.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 90
ya wenye simu nchini wanatumia huduma za fedha za simu, hivyo kama kundi hili
likibadilishwa na wakakubali kuwa wateja wa benki nchini, itaongeza upatikanaji
wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Nuebrand Events
Company, Abdul Ally, akisema kuwa kumekuwa na mafanikia sana toka kampeni hii
ianze kwani idadi ya makampuni washiriki yamekuwa yakiongezeka toka 1200 mwaka
2012 mpaka 3600 kwa mwaka huu. “Mafanikio ni makubwa, tumepata pia washiriki toka
mikoani mfano Mbeya. Hali hii inatutia moyo,” alisema.
Alisema kuwa mwakani uhamasishaji huu utafanyika
pia jijini Arusha ikiwa ni katika mkakati wa kuhakikisha mikoa mbalimbali
inafikiwa na huduma hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...