Mgeni
Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah
Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg.
Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee
hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar
es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
Mwenyekiti
Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa akitoa hotuba
yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya
Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust
Fund,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar
es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee
hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
Katibu
wa Bonnah Education Trust Fund,Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa
ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili
kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa
Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg.
Ramadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani
Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar
Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust
Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni
Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.
Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 15
kutoka kwa Meneja wa Miles Networks International nchini Tanzania,Diana
Paul (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education
Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni
Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.
Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 4.4
kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Resolution
Insurance,Angela Tungaraza (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi
wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...