DSCN1621
Mfugaji wa Heifer International Tanzania Abel Mwakatumbula na mkewe wakiwa na Makamu wa Rais wa shirika hilo Bw. Steve Denne aliyetembelea Tanzania kwa mara kwanza wiki iliyopita kuona miradi inayoendeshwa na shirika hilo. 
Katika ziara hiyo, Steve Denne alitembelea ofisi za mkoa wa Mbeya akifuatana na Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk Henry Njakoi, Meneja Mradi wa EADD Tanzania Bwana Mark Tsoxo, ambapo walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro. 
Katika Mazungumzo yake na Mheshimiwa Abbas Kandoro, Bw Denne aliishukuru sana serekali ya Tanzania kwa mahusiano mazuri na ushirikiano mkubwa kwenye kutekeleza miradi ya shirika hilo nchini na hasa katika kuanzisha Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD). Aliahidi kuwa shirika hilo kupitia mradi wa EADD na miradi mingine tarajiwa, litaendelea kuleta mabadiliko kwa kuwasaidia wafugaji wadogo kwenye mikoa wa Mbeya, Iringa na Njombe ili kuinua uchumi wao na kuwa na ufugaji wenye tija na endelevu.
Pamoja na miradi aliyoitembelea Steve Denne, mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaoanza Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe kijiji cha Kyimo ambapo aligawa mtamba kwa mfugaji wa kikundi cha Faraja kama dira ya shirika hilo ya “Toa Zawadi Pia” – Pass On The Gift.
Akiwa nchini, Makamu wa Rais wa shirika la Heifer International alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa nchini wakiwemo wasindikaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Kassim Gharib Juma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...