Kampuni ya simu za mkononi Airtel inawatangazia wateja wake,
wasanii na wanamuziki kuwa yale mashindano yanayotoa fulsa kwa wenye
vipaji ya Airtel Trace yanazinduliwa rasmi kesho katika viwanja vya Coco
beach jijini Dar es saalam kuanzia saa 12 jioni.
Uzinduzi huu
utawashirikisha wasanii Wakali nchini akiwemo Ommy Dimples pamoja na
kundi zima la ya YAMOTO BAND kwa burudani kabambe kwa umati utakao
jitokeza hapo kesho katika viwanja hivyo.
Akitoa maelezo kuhusu
uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Airtel,Aneth Muga alisema
"tunawakaribisha wateja wetu, wapenzi wa muziki na watanzania kwa
ujumla katika viwanja vya coco beach kesho jumatano ili kushiriki
pamoja nasi katika kusherehekea uzinduzi huu rasmi na kuanza safari ya
kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Tanzania.
Airtel kupitia Trace Music Star inatoa nafasi kwa wapenzi wa muziki na
waimbaji chipukizi kupata dili poa kabisa kwa kurekodi akapela zao
kupitia simu zao za mkononi kwa kipaga na kuimba kaktika namba
0901002233 na hatimae kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo kuingia katika kinyanganyiro cha kuwa super star na mshindi wa
Airtel Trace wa Afrika.
Sambamba na hilo tunapenda kuwatangazia watanzani kuwa namba yetu ya
kukuwezesha kuwa mshindi ya 0901002233 sasa iko wazi, hivyo wanaweza
kurekodi na kutuma nyimbo zao sasa . kwa maelezo zaidi tembelea
tovuti ya www.tracemusicstar.com
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga akitangaza namba
itakayotumika katika mashindano ya Airtel Trace Music kuwa ni
0901002233 PIGA, IMBA , SHINDA na AIRTEL
Kikundi cha yamoto Band wakipasha kwaajili ya kutoa
burudani kesho katika viwanja vya COCO beach kuanzia saa 12 jioni
wakati wa Uzinduzi wa Airtel Trace Music Stars, Kiingilio ni BURE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...