Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imehitimisha wiki hii inayosherehekewa duniani kwa
kuwatembelea wateja wake mbali mbali na kuwashukuru kwa kutumia huduma
na bidhaa zake.
Airtel imetembelea wateja wake katika maeneo mbalimbali ikiwa pamoja
na Tandika, magomeni, Temeke , sinza, Mbagala, illala , kinondoni na
katika maeneo yenye watu wengi na kuongea nao kwa nyakati tofauti
lengo likiwa ni kupata maoni juu ya huduma na pia kuwaelimisha kuhusu
huduma na ofa mbalimbali.
Alikadhalika wakurugenzi wa Airtel walitembelea wateja katika ofisi
zao na kutembelea call center kituo cha kuhudumia wateja waaopiga simu
na kuongea na wateja wanaopiga namba 100 kwa msaada zaidi.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha wiki hii Mkurugenzi wa kitengo cha
huduma kwa wateja Bi Adriana Lyiamba alisema” tumekuwa na wiki ya
mafanikio makubwa kwani tumepata nafasi nzuri ya kuendelea kuonana na
kuongea na wateja wetu ana kwa ana na kuwazawadia ikiwa ni kuwashukuru
kwa kuwa pamoja nasi na kutumia huduma zetu.
Tunaahaidi kuendelea kutoa huduma bora zilizo za kisasa na za kibunifu
huku tukitoa huduma kwa wateja zenye uzoefu tofauti kupitia kituo
chetu cha kupokea simu (call center) maduka yetu na sehemu zote ambazo
wateja wanapata huduma zetu. Tunapomaliza wiki hii maalumu kwa huduma
kwa wateja tunapenda kuwahakikishia watanzania huduma bora kwani
tunatambua huduma bora ni mwendelezo wa maisha ya kila siku na si kwa
wiki hii tu.
Akiongea wakati alipotembelewa ofisini kwake Bwana Aliasger Hussein
Gomberawala alisema” tunafurahi kwa uongozi wa Airtel kuwa nasi leo
hapa, tumekuwa wateja wa Airtel kwa muda na tunafurahishwa na huduma
zao kwa ujumla, matatizo ya kimtandao katika technologia hii yapo
mengine ni ya uelewa wa vifaa vya kisasa na technologia hivyo elimu
inatakiwa kutolewa ili wateja waende sambamba na mabadiliko haya.
Tunaomba Airtel waendelee kutuletea huduma za kibunifu na kuendelea
kupunguza gharama za mawasiliano kwani tunategemea sana haya
mawasiliano katika kuendesha biashara zetu.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba
(katikati), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Kassim Mtingwa (wa
tatu kushoto) na Meneja Uendeshaji Huduma kwa Wateja, Amit Arora
wakikata keki kama ishara ya kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja katika
hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Airtel
kilichopo Quality Centre Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam
jana.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba
(kushoto), akitoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo wakati wa kufunga
Wiki ya Huduma kwa Wateja, katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha
Huduma kwa Wateja cha Airtel kilichopo Barabara ya Nyerere jijini Dar
es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba
(kushoto), akimkabithi kifurushi cha zawadi mteja wake Bwana Aliasger
Hussein wakati Airtel ilipotembelea wateja wake katika wiki ya huduma
kwa wateja.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja
wakiwa na maongezi na Bwana Aliasger Hussein wakati Airtel
ilipomtembelea ofisini kwake katika wiki ya huduma kwa wateja.
pichani ni Meneja huduma kwa wateja Jacob Sumary na Afisa huduma kwa
wateja bi Neifita Olomi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...