KAMPUNI ya simu za mkononi ya airtel imezindua rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya Airtel Trace Music Stars kwa kurekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi huku baadhi ya wasanii chipukizi wakipata nafasi yakuonyesha vipaji vyao katika viwanja vya Coco Beach

Akizungumza katika uzinduzi huo uliopambwa na burudani mbalimbali ikiwemo Yamoto bendi katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es salaam meneja uhusiano wa airtel bw. jackson mmbando amesema kila mtanzania anayo nafasi ya kushiriki katika shindano hilo kwa kupiga simu namba 0901002233.

Aidha Mmbando ameongeza kuwa lengo la kuanzisha shindano hilo ni kuinua vipaji vya watanzania wenye kujua kuimba ili wapate nafasi ya kuwa staa wa kimataifa.

Nae balozi wa shindano hilo Ommy Dimpoz amewaomba watanzania kujitokeze kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi kabambe ikiwemo kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na safari ya kwenda nchini marekani kwa ajili ya kupata mafunzo ya kimuziki na nguli wa muziki wa amerika Akon.
Wasanii wa kundi la yamoto band wakiwa na msanii maarufu nchini ambae pia ni balazo wa airtel trace music stars tanzania Ommy Dimpos wakionyesha namba maalum itakayotumika kupiga na kutuma nyimbo kwa wasanii chipukizi kwenye shindano la airtel trace music stars lililozinduliwa rasmi jana.
Meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando akizindua na kutangaza rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa kukerekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana coco beach.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...