Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake akimtambulisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya maendeleo ya ujenzi ya Detroit Nchini Marekani Bw. Andrew G. McLemore kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipokutana kwa mazungumzo VIP ya Uwanja wa ndege wa Pemba. Aliyepo kushoto na Balozi Seif ni Afisa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh. Suleiman Saleh.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake kwenye uwanja wa ndege wa Pemba.
Meneja wa Kampuni ya Mecco Bwana Abdullkadir Mohamed Bujeti akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa bara bara ya wete gando inayoejngwa na Kampuni hiyo.
Balozi Seif akisalimiana na Mtoto mlemavu anayeishi katika Kijiji cha Gando jina halikupatikana mara moja baada ya kukaguwa ujenzi wa Bara bara ya Wete - Gando inayoendelea kujengwa na Kampuni ya Mecco yenye Makao Makuu yake Nairobi Nchini Kenya.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...