Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (wa pili kushoto) akikabidhi hundi ya sh milioni moja kwa Peter Celestine, mmoja wa washindi wa shindano la  kutafuta na kukuza mawazo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali wakati wa shindano hilo jijini Dar es Salaam jana. Shindano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Tanzania Youth Alliance (Tayoa) kwa udhamini wa benki za NBC na Barclays.Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika na Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa NBC Tanzania, Mussa Jallow.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (wa pili kushoto) akikabidhi hundi ya sh milioni moja kwa Frank Mauggo, mmoja wa washindi wa shindano la  kutafuta na kukuza mawazo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali wakati wa shindano hilo jijini Dar es Salaam jana. Shindano hilo linafanyika kwa udhamini wa benki za NBC na Barclays.Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika.
 Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika (kushoto) akizungumza muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Wateja Binafsi (Consumer Banking) wa Benki ya Barclays Afrika, Rajal Vaidya (wa pili kushoto) kuzindua shindano la  kutafuta na kukuza mawazo ya ujasiriamali kwa vijana liitwalo ‘Vijanatz Business Plan competition’ chini ya udhamini wa benki za NBC na Barclays. 
 Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakiwa kazini wakati baadhi ya washiriki wakitoa mada zao. 
Ujumbe wa benki ya NBC, na Barclays Afrika, washiriki wa shindano la Vijanatz Business Plan na viongozi wa Tayoa wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla hiyo jijini Dar es Salaam jana.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...