Aina hii Malware inayojulikana kama Tyupkin yaleta maafa katika mashine za ATM. Tyupkin imekua ikisambazwa na kundi la wahalifu mtandao kutokea ulaya mashariki na kusababisha pesa nyingi kuweza kutoka kupitia ATM mashine ambapo tayari wataalam wa usalama mitandao kutoka Kaspersky Lab wakishirikiana karibu na polisi wasio na mipaka “Interpol” wameshaanzisha oparesheni ya pamoja kutafuta chanzo na ugunduzi katika mashine 50 umebainika hadi sasa.
Uchunguzi wa kina umeonyesha Mashine zilizo athirika zimekua zikigundulika kuwa na Window XP yenye 32-bit ambayo tayari Microsoft walisha tahadharisha watumiaji wake. Utafiti unaonyesha Mashine nyingi za ATM bado zimeendelea kutumia Window XP ambapo imekua ikirahisisha sana kuingiliwa na wahalifu.
Tahadhari imeendelea kutolewa katika maeneo mengine kwani ingawa kunajitihada za dhati za kukabiliana na Tyupkin bado inaonekana kusambaa katika maeneo mengine mbali mbali duniani na hofu ni kubwa kuwa huenda Afrika ikaonekana kuwa ni eneo jipya litakaloathirika.
Ili kupata kujua zaidi juu ya ya angalizo la Window XP BOFYA HAPA HAPA
Na kupata taarifa za kitaalam za ya Tyupkin
na uchunguzi wake BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...