.jpg)
Na Sultani Kipingo
Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Bi Julia Pierson (pichani) , Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Rais wa Marekani maarufu kama Secret Service, amejiuzuru nafasi hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wan chi hiyo Bw. Jeh Johnson ametangaza leo. Katika taarifa yake Bw. Johnson kasema atamteua Bw. Joseph Clancy kukaimu wadhifa huo nyeti.
Afisa
habari wa Ikulu ya Marekani Bw. Josh Earnest amesema katika mkutano
na wanahabari leo kuwa Rais Barack Obama alimwita Bi Pierson na kumshukuru kwa
utumishi wake katika Idara hiyo na nchi ya Marekani, na kwamba Rais huyo
aliweka bayana kwamba iko haja ya kuwa na uongozi mpya katika Idara hiyo.
Akiongea
baada ya uamuzi huo wa kuachia ngazi, Bi. Pierson alisema ulikuwa ni uamuzi
mchungu. “Nadhani (uamuzi huo) kwa maslahi ya Secret Service na umma wa
Wamarekani. Congress (Bunge) limepoteza
imani name kuongoza Idara hii. Vyombo vya habari navyo vimeweka bayana kuwa
hili ndilo wanalotarajia. Ni uchungu kuacha kazi katika Idara hii ambayo inaandamwa
na kashfa mbalimbali za uwajibikaji mbovu wa usalama”.
Bi Pierson
alikuwa amekalia kuti kavu na kuwekwa katika hali ngumu kufuatia matukio kadhaa
ya kuhatarisha usalama (wa Rais), ikiwa
ni pamoja na mtu mmoja kuruka uzio wa White House na kuingia ndani akiwa na
kisu mkononi mnamo Septemba 19 mwaka huu. Inaripotiwa kuwa aliingia humo ndani
baada ya kumzidi nguvu afisa usalama aliyekuwa lindo, kabla ya kuzidiwa nguvu
na afisa mwingine aliyekuwa amemaliza zamu.
Baada ya
tukio hilo, matukio mengine ya kuhatarisha usalama wa Rais yakaibuka. Moja
likiwa ni kuruhusiwa kwa mtu mmoja aliyewahi kufungwa jela kuingia katika lifti
moja na Rais Obama alipokuwa akizuru Taasisi ya kuzuia magonjwa mwezi uliopita.
Pia kuna tukio la mtu kupiga risasi Ikulu hiyo ya Marekani ambayo pia ni makazi
rasmi ya Rais wa Marekani.
Jumanne iliyopita Bi Pierson aliwekwa kitimoto na kamati ya
Bunge kuhusu matukio hayo. Alisema tukio la karibuni lilikuwa halikubaliki na
akakiri udhaifu wa idara katika majukumu yake. “Nakubali kubeba lawama zote”, alisema. “Haitotokea tena.
Ahhhgh..kawaida hata bongo wanajiuzuru sana tu viongozi wetu ....tena hata bila ya kuwepo shinikizo........
ReplyDeleteusala wa taifa wa marekani michuzi.
ReplyDeleteHuu ndiyo unaitwa uwajibikaji utendaji ukiwa na kasoro katika ofisi yako unatakiwa kujiuzulu hata kama hukushiriki. Hii inasaidiaa wafanyakazi wawe makini kuhamasisha kazi katika ofisi zao.
ReplyDeleteAnonymous 1 unayoyasema ni kweli? How many times watu wanang'ang'ania vitengo japo vinawashinda?Bongo kuachia ngazi,kukubali kushindwa ni SHIDAAA!
ReplyDeleteBongo hakuna uwajibikaji,swala la kujiuziru ni ndoto.
ReplyDelete