Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB, imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya Kamati ya Amani na ushirikiano ikiwa ni maandalizi ya mechi baina ya viongozi wa madhehebu ya dini.

Mtanange wa viongozi hao unatarajiwa kufanyika Oktoba 12, mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya amani duniani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi jezi na hundi ya sh. milioni tano  ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema muungano huo umeonyesha sura ya kushirikiana baina ya madhehebu mbalimbali.

“Nchi mbalimbali zimechafuka kwasababu ya migogoro ya dini, lakini viongozi hawa wameonyesha muungano na sisi wengine tunapaswa kushirikiana na kuvuruga amani kwa imani za dini zetu,”alisema.

Dk. Kimei alivitaja vifaa hivyo ni jezi zenye rangi mbili tofauti, tracksuit ambapo kila jezi zikiwa 40, na kuwapatia hindi y ash. milioni tano kwaajili ya maandalizi.

Aidha alisema CRDB itaendelea kuwa karibu na wateja wake ili kushirikiana nao na kuendeleza huduma.

Mtanange huo utawajumisha Masheikh, Maimamu, Maaskofu, Wachungaji na Mapadre huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum,  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo aliishukuru benki hiyo  na kueleza kuwa lengo la mchezo huo ni kuimarisha amani iendelee kudumu.

Naye Katibu Padre John Solomon, alisema kuwa wameamua kuonyesha mchango wa kuthamini amani na kuepuka mapigano.
Viongozi hao wa dini wameshaanza mazoezi kwajili ya kujiweka tayari kufanya vizuri katika mchezo huo wa kuhamasisha amani na utulivu nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa tatu kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum kwa ajili ya mechi ya viongozi wa Kamati ya Amani na Ushirikiano inayowaunganisha viongozi wa dini zote itakayofanyika Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon (wa pili kulia),  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya Kijitonyama, Lucas Busigazi (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mchungaji George Fupe (wa pili kushoto). 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles kimei akizungumza na waandishi wa habari.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akionyesha jezi namba 9 atakayoitumia katika mchezo huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...