Wadau mbalimbali wakiwasili kwenye hotel ya Millennium Durham tayari kwenye DICOTA 2014 utaonza rasmi Ijumaa Oct 3, 2014 kwenye mji wa Durham jimbo la North Carolina mkutano utamalizika siku ya Jumapili Oct 5, 2014 kwenye picha kushoto ni mpiga picha za kiwango na maarufu kutoka DMV Bi Iska Jojo na makamu wa rais DMV Bi, Harriet Shangarai wakielekea vyumbani baada ya kuwasili kwenye hotel ya Millennium muda si mrefu na kukutana na ukodak wa Vijimambo ambao utakuwepo kwenye mkutano huo kuwakilisha.
 Maafisa wa DICOTA wakihakiki usajili wa wadau waliofika mapema leo siku ya Alhamisi Oct 2, 2014 tayari kwa DICOTA 2014 Convetion.
 Wadau wakifuatilia usajili wao kuhakikisha kila kitu kipo sawa wadau wawili kushoto ni Suleiman Zanangwa na Focus wawakilishi wa Tanzania Ports Authority
Msanii wa vichekesho kutoka kundi la Ze Komedi Masanja mkandamizaji akicheza na simu yake kutupia mawili matatu kwenye mitandao ya kijamii akiwa nae tayari kuwakilisha kwa mara ya kwanza katika historia ya DICOTA ndani ya Durham, North Carolina.

Wawakilishi toka Global Land Solutions toka Tanzania wakipata picha ya kumbukumbu kama walivyokutwa na kamera ya Vijimambo kwa picha zaidi bofya HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...