Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua huduma yao mpya na maalum kwa Watanzania,leo kwenye hoteli ya New Africa,Jijini Dar es salaam.Kulia ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Ronald Baraka Shelukindo na kushoto Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania,Furaha Samalu
Kifurushi hiki kipya cha
Bomba kina chaneli nyingi nzuri ikiwemo chaneli iliyozinduliwa hivi karibuni ya Maisha Magic Swahili
inayoonyesha filamu za kitanzania; chaneli ya Telemundo
inayojulikana kwa michezo ya kuigiza ya kimapenzi ya Amerika ya Kusini pamoja na Nickelodeon na Disney Junior
zinazoonyesha vipindi vya watoto.
Meneja Mkuu wa MultiChoice
Tanzania, Peter Fauel, alisema kuwa kifurushi kipya cha Bomba kitagharimu kiasi cha TSh 17,000 tu kwa
mwezi: " Uzinduzi wa kifurushi hiki cha Bomba ni jambo la furaha na
msisimko sana kwetu, kuona kuwa sasa watanzania wanaweza kupata kifurushi
kinachokidhi mahitaji yao.
Kila wakati, MultiChoice inafanya jitahada za kubuni
namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani. Sasa, watanzania wameongezewa uwanja wa uchaguzi
kwa bei iliyo chini na kiwango cha juu cha burudani ikiwemo filamu, makala, habari,
vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo."
Usikose ofa yetu ya
uzinduzi huu - watakaojiunga watapata DStv ikiwemo gharama ya ufundi kwa TSh 99,000 tu kwa kipindi maalum.
DStv Bomba pia itakuwa na chaneli za Africa
Magic Epic Movies, Discovery World, CBS Action, CBS Reality na CBS Drama pamoja na Select Sport 1 na 2 kwa vipindi vizuri vya
michezo.
SuperSport Select na
SuperSport Select 2 zitaonyesha ligi kuu ya Uingereza, Kombe la klabu bingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Hispania, Ligi
kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi. SuperSport Blitz itawaletea habari
zote za michezo.
Kwa habari zaidi kuhusu
burudani kwa ajili ya familia, tembelea tovuti:
Is it 17000 or 170000 per month?. If the former it is really cheap and cheerful
ReplyDelete