MSANII wa vichekesho kutoka Kenya, Fred Omondi akisaini mkataba wa kufanya onyesho la Siku Ya Msanii katika ofisi za Siku Ya Msanii, Mikocheni Dar es Salaam, pembeni ni Mratibu wa Siku Ya Msanii, Justin Jones Kussaga. Picha zingine ni Erick Omondi


WACHEKESHAJI maarufu kutoka nchini Kenya, Erick Omondi na Fred Omondi wamealikwa kutumbuiza katika Tamasha la Siku Ya Msanii litakalofanyika Jumamosi ijayo kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.



Mratibu wa Siku Ya Msanii, Justin Jones amesema mjini Dar es Salaam kwamba wakenya hao wataungana na wasanii wengine wa muziki wa dansi, taarabu, bongo fleva, ngoma za asili, sarakasi na wanenguaji katika maadhimisho hayo.

“Tumewachukua Erick Omondi na Fred Omondi ambao wanatokea Kenya kwa ajili sanaa za maonyesho ya majukwaani, hawa wataungana na wasanii wengine wa  Tannzania ambao tutawatangaza Jumatatu” alisema.

Alisema lengo la kuwaita wasanii hao wa Kenya ni kutengeneza mshikamano katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kutokana na ukweli kwamba sanaa lengo lake kubwa ni kuunganisha watu huku pia wachekeshaji hao wakiwa wanapendwa zaidi kwa ucheshi wao.

Kwa upande wake  Fred alisema wamefurahi kupata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha hilo kubwa na kwamba watanzania watafurahia kazi yao.

“Mimi na kaka yangu tutakuwepo kuungana na wenzetu wa Tanzania katika kusheherekea Siku hii ya Msanii Duniani, tumefurahi kupata nafasi ya kuburudisha kwenye Siku Ya Msanii Tanzania,” alisema.


Fred alikuwa nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa kutumbuiza katika siku hiyo ambayo itafanyika Mlimani City Dar es Salaam, ambapo kiingilio kimetajwa kuwa sh 70,000 kwa VIP n ash 50, 000 kwa viti vya kawaida.


Siku Ya Msanii Tanzania inaandaliwa na Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo imedhaminiwa na New Habari (2006) LTD kupitia magazeti ya Dimba, Bingwa, Mtanzania na The African, Channel Ten, Magic FM, Michuzi Media, PSPF, Proin Tanzania, Azam Media, CXC, Clouds FM, Ledger Plaza Hotel na EFM.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...