JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA AFYA NA USTAWI WA JAMI.
Kuna taarifa katika vyombo vya habarii liyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA ,kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari kuu ya dawa na kusababishia ukosefu dawa katika baadhi ya hospitali.
Ni kweli bohari kuu ya dawa
imepungukiwa fedha za kununulia dawa , lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa
huduma kabisa kama inavyoelezwa. Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha
fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza
dawa.
Katika kukabiliana na hali hii hospitali zote kupitia waganga
wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia 50 ya mapato yanayotokana na uchangiaji
kwenda bohari kuu ya dawa.
Kuhusu ukosefu wa matibabu katika Taasisi
ya Saratani ocean road, ni kweli kwa
sasa baadhi ya mashine hazifanyi kazi na zinazofanya kazi ni chache hivyo
kuzidiwa wakati fulani.Hatahivyo wizara
imekwisha agiza vifaa hivyo ambavyo ni ghali sana toka Canada na vinategemewa
kufika wakati wowote kuanzia sasa na pia ikumbukwe kuwa matibabu
yanatotolewa bila malipo na gharama zote
ni za serikali.
Wizara kwa sasa imeagizwa katika
mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN)ambapo wataalam wanamalizia kazi za utekelezaji
wa mpango huo. Ambapo pia umezingatia namna ya kukabiliana na jinsi ya kuhakikisha
dawa zinapatikana kwa wakati katika
vituo vya matibabu na kuiboresha zaidi
bohari ya dawa. Baada ya kuanza utekelezaji huo suala
la ukosefu wa dawa na vifaa tiba utapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Pamoja na wizara kupeleka bohari
tyadawa pesa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hospitali zihakikishe
zinapeleka asilimia 50 ya mapato kama zilivyoagizwa na kutokufanya hivyo
kiongozi husika atawajibishwa.
Mwisho wizara inapenda kuwahakikishia
wananchi kwamba dawa na vifaa tiba muhimu vinapelekwa katika vituo vyote , pia
inaendelea kufanya kazi na taasisi zote zisizo za kiserikali kwa karibu kwa
faida ya wananchi wote.
Imetolewa na :-
Dkt. Seif S. rashidi (Mb)
WAZIRI WA
AFYA NA USTAWI WA JAMII
27/10/2014
mbona anazunguka hoja .... hoja ni serikali inadaiwa deni hilo, kwanza wakubali wanadaiwa then ILIPE deni hilo ... maagizo mengine sijui BRN yatafuata baadaye
ReplyDeleteMnachanganya tu wananchi na watendaji wengine wa ngazi za chini.
Ni vizuri serikali imekiri, nilidhani ni taarifa ya kukanusha kumbe kuunga mkono. Huu ndio uwazi.
ReplyDeletesesophy