
Salam nyingi na hongera sana. Katika kuendeleza
libeneke, nami nimeona sina budi kuunga mkono juhudi za kukuza lugha yetu kwa
njia hii. Naomba nitangaze blogu mpya ya kawaida lakini yenye mambo yanayovutia
sana kusoma na kufahamu.
Blogu hii
itajikita zaidi katika kuelezea mambo mbalimbali kwa muundo mwepesi na kwa
Kiswahili ili kukuza uelewa wa mambo mengi katika jamii yetu ambayo yameachwa
katika lugha ngumu za kisayansi na hivyo kuwanyima fursa watu wengi kuyafahamu
kiundani. Hivyo tutakuwa tukitoa
uchambuzi wa mambo na “updates” au taarifa katika nyanja za sayansi, saikolojia na elimu nyingine zenye kuvutia
sana.
Ni matumaini yangu kwamba kupitia blog hii, wakubwa kwa wadogo watajifunza na
pia kuchangia elimu mbalimbali zitakazowagusa au kuwavutia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...