https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNCFTKDU_zdlR7r2Na3QmWrnM9_L7GufZ8mvjGXWGPwn-mfmvkCauNiTy2vP_ixGjSKVL9H-m_S7GxMZVeXgoQ0KCydXjLas2-NUnXXQmq51O7u7ENQ4S5BqpjgeKniafnEYNaNw/s640/RPC+NJOMBE.JPG
Jeshi la polisi mkoani Njombe limeamua kuchukua uamuzi mgumu wa kuwafukuza kazi askari polisi wake watatu kwa makosa mbalimbali waliyoyafanya ikiwemo vitendo vibaya kinyume na sheria za jeshi hilo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa mtandao huu na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani (pichani) askari hao waliofukuzwa kazi ni EX.G. 3172 PC Ramadhani Iddi Saidi, EX.G. 9693 PC Emmanuel Morson Lyimo pamoja na EX.G. PC Miraji Jumanne Mtea

Kamanda Ngonyani amesema Jeshi la polisi limeamua kutoa adhabu hiyo kali kutokana na vitendo mbalimbali vya utovu wa nidhamu walivyovifanya ikiwemo tukio la hivi karibuni la kupigana hadharani Septemba 2 mwaka huu Mjini Njombe

Amesema wanategemea adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa askari wengine wenye tabia kama hiyo kwani jeshi halitawavumilia askari wake ambao wanakwenda kinyume cha sheria

Katika hatua nyingine Kamanda Ngonyani amewataka wananchi kuwa makini na askari hao waliofukuzwa kazi huku akisisitiza wananchi kutambua kuwa askari hao si watumishi tena kuanzia Oktoba 24, mwaka huu

Na Edwin Moshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Napenda kukupongeza Kamanda Ngonyani kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu ya Taifa. Katika hilo la Wananchi kuwa makini na wafukuzwa hao mimi binafsi naona ingekuwa sahihi kama Kamanda ungechukuwa hatua za kutoa either katika mtamdao huu au katika magazeti picha zinazoonesha sura za wahusika hao ili tuweze kuwajua na kuchukua tahadhari hizo. Daima mbele hapana kuogopa Kamanda. Unalo jukumu la Wananchi nyuma yako. Hongera sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...