Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Wananchi wakifurahia hotuba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
Sehemu ya barabara ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam
![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. PICHA NA IKULU Picha zaidi BOFYA HAPA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, amezindua rasmi Barabara ya Kisasa ya
Mwenge-Tegeta ambayo ni sehemu ya Barabara ya New Bagamoyo Road, mjini Dar Es
Salaam.
|
Barabara
hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha
ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa
la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi
wa Barabara hiyo.
Rais
Kikwete amefanya uzinduzi huo katika eneo la Makutano ya Kambi ya Jeshi ya
Lugalo na Barabara ya Kawe katika sherehe iliyoshuhudiwa na mamia ya wananchi.
Alikuwa ni Rais Kikwete ambaye aliweke jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara
hiyo Aprili 4, mwaka 2011.
Barabara
hiyo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa Barabara itokayo Makutano ya Barabara ya
Kawawa, Kinondoni hadi Tegeta. Ujenzi wa awamu ya pili wa kilomita 4.3 kati ya
Mwenge na Makutano ya Barabara ya Kawawa, unatarajiwa kuanza wakati wowote
baada ya mipango yote ya ujenzi huo kukamilika.
Barabara
hiyo ya Mwenge-Tegeta inalenga kupunguza msongamano wa magari katika eneo la
kaskazini mwa Dar Es Salaam na pia ni sehemu ya bararaba kuu inayounganisha
Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani, kupitia Wilaya ya Bagamoyo, na
kuunganisha mikoa hiyo na mikoa ya kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza
kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa Barabara hiyo iliyojengwa na Kampuni ya
Konoike kutoka pia Japan, Balozi wa Japan katika Tanzania, Mheshimiwa Masaki
Okada amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulichelewa kukamilika mwaka jana,
kama ilivyopangwa, kwa sababu ya wajenzi kukabiliwa na matatizo ya mafuriko
makubwa yaliyotokea mwaka 2011.
Mbali
na kutaja misaada mingi katika sekta ya miundombinu na hasa barabara ambayo
imefadhiliwa na Japan katika miaka mingi iliyopita, Mheshimiwa Okada amesema
kuwa Japan sasa iko tayari kuanza ujenzi wa Barabara ya Gerezani-Bendera Tatu,
Dar Es Salaam, utakaogharimu Sh. bilioni 18.5, msaada kutoka Japan.
Aidha,
Balozi huyo amewaomba radhi Watanzania kutokana na ucheleweshaji wa kuanza kwa
ujenzi wa barabara ya juu kwa juu –flyover-
katika eneo la TAZARA, Dar Es Salaam, ambao utagharimu Sh. bilioni 53 ambazo
zinatolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la
JICA.
Amesema
kuwa ujenzi huo umechelewa kwa sababu makandarasi wa Kijapan ambao walitakiwa
kujenga flyover hiyo wanakabiliwa na
kazi nyingi huko nyumbani za kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko
na kimbunga cha Great East Japan
Earthquake and Tsunami, kilichotokea Machi 2011 na kusababisha uharibifu mkubwa
mno.
Aidha,
amesema kuwa wajenzi hao pia wanalazimika kufanya kazi usiku na mchana ili
kukamilisha miundombinu ya kuiwezesha Japan kuandaa Michezo ya Olimpiki ambayo
imepangwa kufanyika nchini humo mwaka 2020.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2014.
Wana CCM na Wana CHADEMA wakifurahia kwa pamoja uzinduzi wa barabara hiyo Tanzania kwanza!! |
Hongera serikali na mheshimiwa mbunge wa jimbo hili pia kwa kufanikisha upanuzi wa barabara hii.
ReplyDeleteMh nafikiri hii ni trunk road. So sidhani kama Mbunge anahusika. Ila swali langu si Magufuli aliwahi kuikataa sasa imekuwa bora? Au ndio changa la macho kama Kilwa Road
ReplyDeleteUkiongeza na picha mbili hizo za watanzania wa vyama mbali mbali wanaocheza ngoma ya kufurahia maendeleo zinanifanya nijivunie kuwa mtanzania.
ReplyDeleteMbunge hahusiki kwa lolote hapo
ReplyDeleteAnahusika au hausiki! so what? Acha fikra mgando! au wewe ndio unahusika!
ReplyDeleteLinapokuja swala la taifa, hasa pale mkuu wa nchi akawa anahusika, kuwa na adabu na heshima! Hakuna barabara ya chama cha siasa, ila kuna barabara ya wananchi na raia kwa ujumla wake!
Don't divide people! President of Tanzania Hon. Jakaya Mrisho Kikwete is the special president! He knows how to live with his people! I am very proud of him! Long live Mr. President!