Wachezaji wa Kagera Walio chini ya Miaka 15 wakishangilia baada ya mpira kumalizika kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Geita kwenye Mashindano ya Copa Coca Cola, Mchezo uliochezwa leo Jumapili 12.10.2014. Kagera wameifunga Geita Bao 2-0. |
Na Faustine Ruta, Bukoba
Kagera wameanza vyema Mashindano ya soka kwa vijana walio chini ya miaka 15, Copa Coca Cola, Leo Jumapili 12.10.2014 Asubuhi baada ya kuichapa Timu ya Geita bao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyumbani Kaitaba.
Bao za Kagera zimefungwa kipindi cha kwanza na cha pili. Bao la kwanza limefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 28 na Avith Frolian aliyekuwa amevalia jezi namba 10. Na bao la pili lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 61 na Kepteni wao Patrick Amos baada ya Kagera kupiga kona na Kepteni wake kuruka juu na kufunga kwa kichwa. Kagera watarudiana na Geita kwao jumamosi tarehe 18 wiki ijayo.
Mchezaji wa Kagera akiendesha...Mashambulizi kwa timu ya Geita leo jumapili Asubuhi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...