Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akielekeza jambo wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakiangalia namna maji yanavyotolewa chini kwa ajili ya kuweka nguzo za Daraja la Kigamboni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...