Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara, Uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mufindi Kaskazini, Iringa, ikiwa ni mwendelezo wa kuiamarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana aliwataka viongozi kutokuwa na tamaa ya kuwa kiongozi na wakati huo huo kutaka kuwa matajiri pia aliwataka kuacha kujipendelea kujipa tenda badala ya kuwapatia kwanza wananchi.
 Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamoud Mgimwa akihutubia na kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga leo.
 Kinana akiangalia mashine za kupasua mbao katika kiwanda cha mtu binafsi cha Emanuel, mjini Mafinga, Mufindi.
 Kinana akiwa na mkurugenzi wa kiwanda binafsi cha mbao cha Emanuel, Charles Akyoo alipotembelea kiwanda hicho leo.
 Kinana akitembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mufindi Kaskazini. Picha zaidi BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...