Na Sultani Kipingo
Yaani ni kama kwamba kubadilika kimchezo kwa  kipa wa Man U David de Gea kutoka kuwa mchekea hadi mmoja wa makipa bora wa ligi kuu ya Uingereza kumekamilika. De Gea, hapana shaka, leo amedhihirisha kuwa mmoja wa walinda mlango hodari, tofauti na na msimu uliopita alipookuwa chini ya kocha David Moyes. Leo Mhispania huyu ameokoa penati na kupangua mipira kibao kumyima Mzee Arsene Wenge na Arsenal yake pointi 2 na kumuokoa kocha mpya Louis van Gaal kutoka katika kuti kavu
Ngoma ilikuwa nzito toka kipyenga cha kwanza.  Ulikuja pale  Cesc Fabregas alipotoa pande tamu kwa Diego Costa ambae alipiga bao moja tamu sana. Kofi la uso kwa mashabiki walioanza kumbeza. Hata hivyo jambo ambalo lingempa hofu Wenger na timu zote zingine ni kwamba leo Chelsea wametandaza kabumbu lisilo la kawaida, na kuhakikisha kuwa hio sio timu ya mtu mmoja. Naam, Costa alifunga tena, lakini hakuwa akihitajika sana. Maana ngoma aliyopiga Eden Hazard si ya kawaida kiasi hata Costa asingefunga, bado tu Chelsea wangepata mabao kwa njia zingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...