Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia)
akiwakabidhi rasmi vijana wa kundi la”WAKALI SISI”la kiwalani jijini Dar es
Salaam simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka,ambazo ni moja kati ya zawadi
walizojishindia katika fainali za
shindano la Dance 100% hivi karibuni na kujishindia kitita cha Tsh Milioni 5 na simu hizo zimeunganishwa na mtandao
wa Vodacom Tanzania muda wa maongezi
kiasi cha shilingi laki moja.
Mabingwa
wa shindano la Dance 100% 2014” WAKALI SISI”wakimsikiliza kwa makini Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu(kulia) wakati alipokuwa akiwahusia kuhusiana na matumizi
mazuri ya simu baada ya kuwakabidhi
rasmi ya simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na Vodacom na
muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi
laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano
hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na kitita cha
shilingi milioni 5.
Kiongozi
wa kundi la”WAKALI SISI” la Kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka
Kambona(kushoto) akipokea mfuko wenye simu aina ya Vodafone Smart Kicka
zilizounganishwa na mtandao huo na kuwekewa muda wa maogezi wa shilingi laki
moja toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ikiwa
ni kati ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano la Dance 100% hivi
karibuni na kuondoka na kitita cha Tsh
Milioni 5.
Mabingwa wa Dance 100% 2014”WAKALI SISI ”wa Kiwalani jijini Dar es Salaam,wakionesha
simu aina ya Vodafone Smart Kicka zikiwa na muda wa maongezi wa shilingi laki
moja mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia)kundi hilo liliibuka
mshindi wa kwanza katika fainali ya
shindano hilo hivi karibuni ambapo walijinyakulia kitita cha shilingi milioni
5.
Kundi la”WAKALI SISI”ambalo ni mabingwa wa
shindano la Dance 100% 2014 wakionesha makali yao ya kucheza dansi katika makao
makuu ya Vodacom walipofika katika hafla fupi yakukabidhiwa rasmi ya simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka
zilizounganishwa na muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi laki moja ambazo ni moja ya zawadi
walizojishindia katika fainali ya shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza
na kujizolea kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni5.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...