Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na anawakilisha kama Gavana Mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. Katika picha viongozi hao wakiwa wanafanya majumuisho ya majadiliano ya awali na kukubaliana cha kufanya kwa pamoja na viongozi kutoka IMF na WB kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile hayupo katika picha, alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.

Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.Wakichukua mapendekezo kutoka kwa viongozi wa IMF na WB hawapo kwenye picha. Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania akiwa amefuatana na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kulia ni Bw. Philip Mpango Katibu Mtendaji tume ya Mipango akifuatiwa na Msaidizi wa kamishna sera Bw. Shogholo Msangi na wa mwisho ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na walioketi nyuma wote ni wajumbe kutoka Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...