Timu kongwe visiwani Zanzibar Jamhuri ya Wete Pemba iliyoanzishwa mwaka 1954 imepokea vifaa mbali mbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 8 kutoka kwa Bw.Suleiman Saleh ambaye alimkabidhi mdaada huo. Mjini Wete Pemba jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba.

Bw..Saleh ambaye ni Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC alikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo viatu.mipira .nyavu za magoli na vifaa mbali mbali vya mazoezi ili kuihamasisha timu hiyo ambayo mwaka ,2003 walikuwa mabingwa Zanzibar na miaka ya 2008 na 2011 ilishiriki katika klabu bingwa Afrika ambapo ilitolewa na St.George ya Ethiopia na Hangwe FC ya Zimbabwe. Katika kujiwekea malengo ys kucheza tena kimataifa katika miaka mitatu ijayo Jamhuri inayoundwa na vijana wadogo imeandaa mkakati maalum kukamilisha azma yao hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...