Wafanyabiashara ndogondogo (MACHINGA), wakiendelea kufanya biashara zao kama walivyokutwa na mpiga picha wetu kwenye kituo cha daladala ubungo na pembezoni mwa barabara jijini ya Morogoro jijini Dar es Salaam, hivyo kusababisha kero kwa watumiaji wa barabara hiyo,eneo hilo lilipigwa marufuku kwa shughuli za aina yoyote na Mansipaa ya Kinondoni lakini jamaa kama wamekaidi amri ile halali kabisa.Picha na Philemon Solomon,Globu ya Jamii.
Home
Unlabelled
mambo yazidi kunoga stendi ndogo ya mabasi Ubungo jijini Dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sasa kama serikari haitujengei mabanda tufanyeje ? Tulale njaa ?
ReplyDeleteTatizo sio Serikali kujengea watu mabanda Kama mtu hatakiwi hapo fuata sheria, muda umefika Jiji letu Kuwa safi cha kufanya Mie naona wanajeshi wanakula pesa za bure waanze kuwekwa mtaani Kuwa security na kuhakikisha usafi wa Jiji na Ulinzi Kuwepo kuwe kusafi na salama wale mgambo hakuna wanachofanya.
ReplyDeleteHacheni onoko nyie, hawa wangekuwa ni baba / mama au ndugu zenu na mnawategemea kula au kulipa ada za shule kutokana na hizo biashara je mngewatoa kwenye webusite kwa kejeri? Au kwakuwa mshajiona mna pesa mnawaona wanachafua mazingira? Watz wenzangu Hacheni kabisa kukufuru Mungu na mshukuru Mungu kwa kidogo mlicho nacho.
ReplyDeleteIngekuwa vyema mngeanzisha mada ya kuona kipi kifanyike kuwasaida hawa vijana na kama Machinga Complex wanaiona sio maeneo mazuri ya kufanyia biashara tufanye nini?
Mbona ata Ulaya, US issue hizi zipo? Mnashangaa Tz??, Wapeni vijana mitaji na maeneo bora wafanye biashara zao.
hivi mnajua Microeconomics ina stimulate uchumi kwa haraka sana na kuwasaidia walio wengi kwa mtu mmoja mmoja na kuondoa umasikini kwa raia walio wengi?! Mngeshukuru wanaisaidia Serikali badala ya kuponda kwa kejeri.
Mdau kutoka Crenshaw County, Alabama.
Joseph
LL.M
Hahahahaaa mdau Joseph LL.M (hii ni jina ama usomi wa sheria?) umechamka na mahasira yako ( ya bills au?) . Nimegugo mji unaodai unaishi sijaona mahali penye uvunjifu wa sheria (LL.M?) sasa sijua unavowasemea mbovu waleta habari tukueleweje...Ankal na timu yako piga mzigo tu, achaneni na hao kina Joseph "LL.M" ambao kila kitu kwao sio sawa. Yaani kaniudhi kweli huyo jamaa, sijui kwa nini maoni yake mmeyaruhusu humu maana yanachafua hali ya hewa. Angekuwa mume wangu leo asingerudi nyumbani, hana hata haya!
ReplyDeleteWe dada unayemponda LL,M upo nchi gani? Nimevutiwa na pozi zako. Uko so sexy na uandishi wako.
ReplyDeleteUsimamizi mbaya wa tunachokianzisha. Wamachinga walishaondolewa hapo, sasa Ni nani aliyewarudisha hapo? Wahusika mpo kimya mnaangalia Tu, mizizi ikiota, mtatumia nguvu kubwa Sana kuin'goa. Ni vema mkaanza sasa kuwaindoa hao watu sasa.
ReplyDeleteMdau hapo juu usimponde mwenzako ili mradi uponde, Crenshaw County, Alabama ipo na ni county iliyopo ndani ya Alabama ebu google vizuri au jaribu kutembea uione dunia na sio kukurupuka tu. Na ata hapa biashara kama hizo zipo na wameruhusu (open market au panaitwa market place)
ReplyDeleteMdau Joseph alichofanya ni kuelimisha kidogo walio nacho wengi wasijisahau pale wanapowaona wasionacho wakitafuta riziki na kuwaona uchafu au takataka.
Na LLM ni Master of Laws na wala sio jina lake, vile nikisema dharau bado inaonesha watz wengi tunayo ambapo unasema jamaa kachanganyikiwa kwa bills, hivi ndugu watz wenzangu mnadhani walio wengi huko nje wana shida sana na bills au maisha yao SIO mazuri saaaana?
Binadamu aliyekamilika ni yule anayekaa chini na kusema 'dah hapa kweli nimekosea au dah asante sana kwa ushauri na nitaufanyia kazi'
LL,M hivi wewe unawasaidia hawa ndg zetu au unafurahia wanavyokauka pale Ubungo na sehemu zingine! Nadhani ungetafakari kwa kina jinsi hao wanavyoumia na ni vipi wasaidiwe (sio mitaji) kwa mawazo ili waweze kunufaika na kazi wanayoifanya na pia kuweza kuisaidia serekali kupata manufaa kutokana na nguvu kazi yao. Hiyo huruma unayoionyesha ni sawa na kuongeza petrol kwenye moto unaowaka. Hao tumewaona muda mrefu na tunakaa nao, maisha yao ni ya shida. Kama hii biashara inalipa basi waende Machinga complex ili serikali iwatambue na ifaidike na mapato yatokanayo na biashara hiyo.
ReplyDeleteHivi nyie tukisema kila mtu afanye anachotaka huu utakuwa ni mji au, hakuna kitu kinakera kama hao wamachinga kupanga bidhaa barabarani, huu mji una watu wengi ile mbaya utakuta mtu kapanga bidhaa zake hata hajali wapita kwa miguuu wanapita wapi, wanasababisha msongamano mkubwa njiani mkiwa mnapishana kisa wamepanga biashara zao sasa ole wako ukanyage hata kwa bahati mbaya, Utakoma Uhuru wa mtembea kwa miguu uko wapi nawauliza nyie mnaosimamia sheria, Thanks God hata hii Ebola isije huku kwetu maana njiani kupita ni kusuguana tu, hutembei kwa raha mara umemgusa huyu mara umegongana na huyu kisa wamachinga nachukia sana hii hali, Kama kila mtu akiachwa afanye biashara zake tu kwa kisingizio wanatafuta riziki iko siku watakuja kupanga hadi kati kati ya barabara na asiwepo mtu wa kukemea hili si wanatafuta riziki!!!! Mji hauleweki kila sehemu ni Biashara ndogondogo kuanzia Posta hadi Ubungo pa kukanyaga ni shida. Hao wanaosimamia sheria kila siku wako Nchi za Watu hawaoni Miji ya watu ilivyo. Tunatia Aibu tubadilike Mji mchafu, Cha kusikitisha kingine ukipita maeneo wanapofanya biashara ndogondogo utaona zinanuka Mikojo na harufu za ajabu wala hawahangaiki kutafuta vyoo wanachofanya wanajibanza kwenye meza zao au mabanda yao wanajisaidia hapo hapo walivyokosa aibu na utu. Maeneo yao huwa ni Machafu mno. Jamani mnaohusika na hili suala acheni Siasa simamieni huu Mji Ipasavyo.
ReplyDeleteHii itakuwa LL.M ya kujamba, maana arguments zako hazifanana na LL.M ninayo ijua mimi Ndugu Joseph.
ReplyDelete