Katika
mkutano muhimu uliofanyika jioni hii hapa mjini Washington DC. Kati ya
ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H.
Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi
namba 1 la Afrika pamoja na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua
nafasi hiyo ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza
mambo muhimu ambayo Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu.
Katika
mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza viongozi wa Benki ya Dunia
kuwa ,anashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya
Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana Tanzania katika kupiga hatua
kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile alisema kuwa pamoja na
kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo ambalo lina
sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti.
Hili
amelieleza kuwa linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo
yanayohusu IPTL kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye
makubaliano. “ IPTL haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili
limeingia katikati hii inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema.
Aidha
aliendela kueleza kuwa sera ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la
Kimasai limetengwa na hivyo kutaka baadhi ya miradi isiende sehemu
nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni changamoto nyingine”. Katika
mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa
ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo.
Kwa
mapendekezo haya mawili makubwa kama yatafikishwa kwenye ngazi ya juu
na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua kama ilivyojipangia.
Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono miwili na
wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi. Hali ya hewa mjini hapa ni ya
baridi na manyunyu ya hapa na pale.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye
ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika
na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo.
Bw.
Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake
wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua
nafasi hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha
mapendekezo yake kuhusu hali halisi ya misaada.
Ujumbe
kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa
akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na
Bw. Peter Larose Mkurugenzi Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakiwaangalia kwa mshangao
wakurugenzi hao wawili walipokuwa wakiingia (hawapo kwenye
picha).habari/picha na Ingiahedi Mduma,Wizara ya Fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...