Meneja wa mradi wa CIRDA kutoka UNDP, Bonizella Biagini akizungumza wakati akitambulisha maofisa waliokuwepo katika uzinduzi wa warsha ya siku tatu ya kimataifa ya ukusanyaji na matumizi ya taarifa ya hali ya hewa kwa nchi 12 duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Mipango ya maendeleo duniani (UNDP) Phillippe Poinsot, Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi.
Na Mwandishi wetu
MATAIFA 11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.
Mataifa hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
Nchi zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin, Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao Tome and Principe,Uganda na Zambia.
Mpango wa CIRDA unafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) na Least Developed Country Fund (LDCF) ukilenga kuwezesha utumiaji wa teknolojia mpya miongoni mwa wakulima, watunga sera na sekta binafsi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP,Phillippe Poinsot Mpango wa CIRDA, ambao ni mfano wa kuigwa kwa juhudi za mataifa ya Afrika ya kuwa na ubadilishanaji wa maarifa na taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, huzingatia uhusishaji wa sekta binafsi, matumizi ya simu na takwimu za kilimo (agricultural index insurance).
Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa rais, mazingira Binilith Mahenge, Ofisa anayeshughulikia mradi huo nchini Richard Muyungi alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo dunia nzima iko katika changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...