Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kushoto) akijadiliana jambo
na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekeleza wa Miradi (PDB)
inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa (wa pili
kulia) mara baada ya kuhudhuria hivi karibuni maabara inayochambua miradi ya afya
itakayoingia katika BRN. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Bw. Mahmoud
Thabit Kombo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt, Mohammed Saleh
Jidawi (kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa), Hawa Ghasia akijadiliana
jambo na Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Bw. Mahmoud Thabit Kombo wakati
viongozi hao walipotembelea maabara inayochambua miradi ya afya itakayoingia katika
BRN.
Baadhi ya wawakilishi wa Wabia wa Maendeleo waliopo nchini wakifuatilia majadiliano
jana jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea maabara ambayo inachambua miradi ya
sekta ya afya itakayoingizwa katika BRN.
Badhi ya washiriki wa maabara inayojadili miradi ya afya itakayoingizwa katika BRN
wakifurahia zawadi waliyopewa na Waziri wa Afya (hayuko pichani) baada ya kundi
lao kushinda katika uwasilishaji wa miradi ya afya itakayochambuliwa zaidi ili kuingia
katika BRN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...