Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti  akizungumza jambo wakati akifungua kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
Maafisa habari mbalimbali kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa kutoa taarifa kwa wananchi.
Kongamano hilo linafuatia matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa.

Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha ya kupata mwaliko. 
 Mwanasheria kutoka Taasisi Kitaifa ya Msaada wa Kisheria (National Organization of Legal Assistance-nola)  Bwana James Malenga akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...