Mwanamuziki kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Kisanii T.I akizungumza na Waandishi wa Habari jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa Sea Cliff hotel jijini Dar kuhusiana na onesho lake la kwanza atakalotumbuiza katika viwanja vya leaders Club,jijini Dar katika tamasha la Fiesta 2014,ambalo hufanyika kila mwaka mara moja,chini ya waandaji bingwa wa burudani hapa nchini kampuni ya Prime Time Promotions Lts sambamba na Clouds Media Group..
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akitoa shukurani za dhati kabisa kwa wadau mbalimbali walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya tamasha la fiesta 2014, ambalo linatarajia kurindima usiku huu katika viwanja vya leaders Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo wasaniii mbalimbali wa ndani na nje pia watatumbuiza jukwaani,aidha kama vile haitoshi Msanii kutoka nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Davido amekiri wazi kuwa atatumbuiza usiku wa leo katika tamasha hilo,bila kikwazo chochote.
 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Kisanii T.I (pichani kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa Sea Cliff hotel jijini Dar kuhusiana na onesho lake la kwanza atakalotumbuiza katika viwanja vya leaders Club,jijini Dar katika tamasha la Fiesta 2014,ambalo hufanyika kila mwaka mara moja,chini ya waandaji bingwa wa burudani hapa  nchini,Kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ikishirikiana na Clouds Media Group.
Mwanamuziki kutoka Nigeria,ajulikanae kwa jina la Davido akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuwa atatumbuiza usiku wa leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 litakalofanyika usiku huu katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar.
Mdau mkubwa wa mwanamuziki T.1 kutoka Dubai ,Rasheed Sazaf a.k.a Sazaf akipeana mkono na Mwanamuziki T.I jioni ya leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...