MWANAMUZIKI wa muziki wa daansi, Tarsis Masela (mwenye miwani), anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yake ya kwanza iitwayo Acha Hizo utakaofanyika Novemba 21 kwenye Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) ulioko  Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini dar leo Masela, ambaye pia ni mwanamuziki na Rais wa bendi ya Akudo, alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo saba na zina ujumbe mbalimbali ambao unalenga kuelimisha jamii.

Masela alizitaja nyimbo zilizoko katika albamu hiyo kuwa ni pamoja na Tabia Mbaya ambayo amemshirikisha ‘Mfalme’ wa taarabu, Mzee Yusuph, Chaguo Langu, Nimevumilia (Lady Jay Dee).

Alisema nyimbo nyingine ni Vidole Vitatu, Penzi Langu Limezidi Asali, Mwiko na Tusiachane.
“Hii ni albamu yangu ya kwanza tangu nianze muziki, nimeshirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na taarabu ili kuifanya iwe na ladha tofauti na ubora wa juu,” alisema Masela.

Aliongeza kuwa katika uzinduzi wake atasindikizwa na wasanii mbalimbali ambao kwa sasa wako kwenye mazungumzo ya mwisho ili kulifanya onyesho hilo liwe na ubora wa aina yake.

Naye Meneja wa msanii huyo, Ray Matata,alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yanaendelea vizuri na wamejipanga kufanya mapinduzi kwenye muziki wa dansi.

Matata alisema kwamba Masela ameonyesha nia na amewataka wadau wa sanaa ya muziki kujiandaa kushuhudia onyesho lenye ubora wa kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...