Jumamosi ya tarehe 4 Mwezi wa Oktoba 2014,wakazi wa ukonga walipata fursa ya kupagaishwa na
burudani ya mziki mnene inayoandaliwa na kituo cha redio cha EFM kwenye ukumbi wa Ukonga
Reaction Centre.
Idadi ya watu wasio hesabika walijitokeza kwa wingi ndani ukumbi huo.
Tuliongea na mmoja wa waandaji wa tamasha hili Dickson Ponella,ambae alisema kuwa mziki mnene
utazunguka Dar Es Salaam nzima na viunga vyake,kama ratiba inavyo elekeza.
“Haina haja ya watu kugombania kuingia ndani,wakumbuke tamasha hili halina kiingilio,ni kwa watu
wote.Tunashukuru kuona baadhi ya watu walio safari kutoka mikoa ya karibu kama vile Morogoro,Tanga
na Mtwara kuja kutushika mkono”,alisema.
Kwa upande mwingine meneja uhusiano wa EFM Kanky Mwaigomole,alisema kuwa wasikilizaji wote
waendelee kusikiliza matangazo yao ili wajue watakuwa wapi na lini.
“Kwakila tamasha hili tuna kipengele kiitwacho kibunda.Huwa tunawaita watu angalau watatu,na
tunawauliza maswali kumi ndani ya dakika moja na mshindi hupewa zawadi mbali mbali,ikiwemo pesa
taslimu”,alisema Mwaigomole.
Meneja uhusiano huyo aliendelea na kusema kuwa tamasha hilo la muziki mnene litaendelea tena
jumamosi ya tarehe 11 mwezi huu wa Oktoba mwaka 2014,huko Kigamboni Navy Beach,Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...