
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima na kupanda mahindi katika shamba kijijini Kwemnyefu Kata ya Mpapayu wilayani Mheza mkoani Tanga pamoja na wananchi wakati alipotembelea shamba hilo na kukagua shughuli za kilimo cha mkono, Katika shughuli hiyo katibu mkuu huyo ameshirikiana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katibu Mkuu huyo kesho anaelekea wilayani Pangani baada ya kumaliza ziara yake wilayani Muheza leo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...