Sehemu ya mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, baada ya kupiga mwereka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani bila ya tahadhari.
Awali, Lori hilo pamoja na kupiga kwake mwereka halikufanya na madhara yeyote wala dalili ya kusema litawaka moto.  Ila baada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafuta yaliyokuwemo kwenye lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza kabisa lori hilo.
Haijafahamika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliyepoteza maisha katika moto huo, ila hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na eneo la tukio  ambazo zimeteketea kwa moto. Nyumba moja ni ya makazi ya watu, ingine ni duka la juma la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni. Globu ya jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo na tutaendele kujuzana.
Sehemu ya Lori hilo likiwa limeteketea kabisa.
Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.
Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Magari ya mafuta yakilipuka ni hatari kubwa kuwa karibu na eneo hilo,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...