 |
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD)
sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko enzi za uhai wake
akiwa katika moja ya semina alizohudhuria.
MTANGAZAJI
na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Ben
Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika
hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora
ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki
mbili.
MUNGU
ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA,
AMIN
|
 |
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD)
sasa TBC, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kikoakizungumza na
Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga
alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo mkoani Tabora wakati wa
uhai wake. |
|
|
|
atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.
R.i.p Ben Kiko
ReplyDeleteR.I.P Ben Kiko hakika sitakusahau kwa jinsi ulivyo tuhabarisha ita vya Kagera 1978-1979 kwa weledi wa hali ya juu
ReplyDeletemungu ailaze roho yako peponi
ReplyDeleteR.I.P Ben Kiko.
ReplyDeleteTutakukumbuka kwa utangazaji wako mahiri na machachari hasa kwenye kipindi cha majira.
Eh kwa sisi wa zamani enzi za RTD tulikuwa tunapenda sana kukusikiliza jinsi ulivyokuwa unahabarisha na kutufurahisha kwa wakati mmoja.
ReplyDeleteMaana utangazaji wa marehemu Ben Kiko ulikuwa wa aina yake peke yake, ukiwa umenuna utacheka tu.
RIP Ben umetangulia na sisi tuko nyuma.
Duh jembe limepotea jina la bwana lihimidiwe
ReplyDelete