
Hivi karibuni kumezuka taarifa za upotoshaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah, Mkurugenzi wa Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima (Honorary Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong.
Watoa taarifa hizo, hawakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao zaidi ya kutoa picha mbalimbali za Bw.Salaah kutoka kwenye mitandao mingine ya kijamii.
Taarifa hizo sio za kweli.
Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za mahusiano ya kidiplomasia ya China, nafasi ya Konseli wa Heshima haitambuliki 'mainland' China.
Kwa maneno mengine hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuteua mtu kuwa Konseli wa Heshima katika eneo lolote la China isipokuwa Hong Kong ambako kuna mamlaka huru za utawala zinazofuata sheria zake.
Kwa maneno mengine hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuteua mtu kuwa Konseli wa Heshima katika eneo lolote la China isipokuwa Hong Kong ambako kuna mamlaka huru za utawala zinazofuata sheria zake.
Kwa faida ya umma, ni vema kufafanua kwamba Nchi ya China inakubali nchi za Nje kufungua Ubalozi kamili (Embassy) ambao makao yake yanatakiwa kuwepo katika mji Mkuu wa China- Beijing na Konseli Kuu ama kwa lugha iliyozoeleka Ubalozi Mdogo (General Consulate) ambao unaweza kufunguliwa kwenye makao Makuu ya mji wowote ule katika Majimbo ya China.
Watu wengi wamekuwa wakichanganya Ubalozi Mdogo au Konseli Kuu (General Consulate) na Konseli (Ubalozi) wa Heshima (Honorary Consulate). Konseli Kuu (General Consulate) ni sehemu ya Ubalozi (ndio maana wengi huuita Ubalozi Mdogo) ambapo kiongozi wake na maafisa wake wote ni watumishi wa Serikali kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Masharti ya kuwa Mkuu wa Konseli 'General Consulate' lazima uwe Afisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje mwenye uzoefu usiopungua miaka 10 ya Utumishi katika Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa muktadha huo, taarifa kwamba Bw.Salaah ameteuliwa kuwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko Guangzhou sio kweli kwasababu Sheria za China haziruhusu uwepo wa nafasi hiyo. Aidha, Bw Salaah hawezi kuwa Balozi Mdogo (Consul General) kwa kuwa yeye sio mwajiriwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hivyo habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na zinalenga kuupotosha umma.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MAMBO YA
WIZARA YA MAMBO YA
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
OCTOBER 30, 2014
Wachongaji tulieni na ni vyema kua mmepata somo. Msiongee tena mkome kuzusha jambo ambalo hamlijui wala halipo... tujaribu kuzungumzia masuala muhimu ya kujenga taifa..
ReplyDeleteWaandishi wa habari wengi wanaofuata sharia, na wengine wachache hubwatuka kufuata akili zake zinavyomtuma na misimamo yao. Naamini hao wachache wakishitakiwa na kutupwa Keko, kesho hawataandika kitu bila kukichunguza.
ReplyDeleteHapo serikali imefanya safii, maana ingekaa kimya ingetuacha wengi na duku duku nyingi vichwani mwetu.
ReplyDelete*Mmbongo Diaspora Daima*
ahsanteeeee kaka
ReplyDeleteUhuru wa vyombo vya habari tanzania ni kupotosha uma, serikali iweke sheria kama chombo kikipotosha uma kushitakuwe ili iwe fundisho
ReplyDeleteKuna waandishi wana chuki na serkali
ReplyDelete