President Xi Jinping of China welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the Great Hall of the People in Beijing this evening during the official formal reception at the climax of the State visit at the invitation of the Chinese leader.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph with their host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan shortly after they arrived for an official formal reception at the Great Hall of the People in Beijing this evening.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph welcomed by their host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete introduces former OAU/AU Secretary General Salim Ahmed Salim to China’s President Xi Jinping during the formal reception held at the Great Hall of the People in Beijing this evening.Left is the Minister for Foreign Affairs Mr Bernard Membe and second left is CCM Secretary General Abdulrahman Kinana.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and his host Chinese President Xi Jinping inspects a guard of honor mounted China’s People Defense force in Beijing this evening during a formal reception at the Great Hall of the people. President Kikwete is on a State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping..jpg)
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his host President Xi Jinping waves to the cheering crowd during a formal reception for the President and his delegation held at the Great Hall of the People in Beijing at the climax of his State visit today..jpg)
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete introduces former OAU/AU Secretary General Salim Ahmed Salim to China’s President Xi Jinping during the formal reception held at the Great Hall of the People in Beijing this evening.Left is the Minister for Foreign Affairs Mr Bernard Membe and second left is CCM Secretary General Abdulrahman Kinana.
China
yamwaga neema kubwa kwa Tanzania
Jamhuri
ya Watu wa China leo, Ijumaa, Oktoba 24, 2014, imetangaza neema kubwa kwa
Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa dola za Marekani milioni 85 kwa ajili ya
shughuli za maendeleo na kuisaidia Tanzania kufanya mageuzi ya viwanda.
Neema
hiyo ya China kwa Tanzania imetangazwa na Rais Xi Jinping wa nchi hiyo katika
mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati yake na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
ambaye yuko katika ziara rasmi ya siku sita katika China.
Mazungumzo
hayo kwenye Jumba la The Great Hall of the People yamefanyika baada ya Rais
Kikwete kukaribishwa rasmi katika Jamhuri ya Watu wa China kwa kupokelewa na
Rais Xi Jinping katika eneo la East Plaza ya Jumba hilo.
Katika
mapokezi hayo ya kuvutia na kusisimua, Rais Kikwete amepigiwa mizinga 21 na
kukagua gwaride la ukakamavu la Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China la
People’s Liberation Army.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Xi Jinping alitangaza kuwa China itaipatia Tanzania kiasi
cha dola milioni 85 ikiwa ni mchanganyiko wa msaada na mkopo usiokuwa na riba,
fedha ambazo Tanzania itaamua yenyewe jinsi gani ya kuzitumia.
“Katika
kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya wananchi
wake, napenda kutangaza kuwa Jamhuri ya Watu wa China itatoa kiasi cha RMB
milioni 200 ikiwa ni msaada na RMB 200 milioni nyingine zikiwa ni mkopo
usiokuwa na riba kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiasi cha
RMB 100 milioni za msaada kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo
zitatumika kwa kadri Serikali hizo mbili zitakavyoamua,”
amesema Rais Jinping.
Rais
huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi hiyo itaisaidia Tanzania katika
uendelezaji wa maeneo ya uwekezaji ya EPZ, uendelezaji wa miundombinu,
itaharakisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na itaingia katika shughuli za
kutafuta gesi na mafuta katika ukanda wa Bahari ya Hindi katika eneo la
Tanzania.
Rais
Jinping pia ametangaza kuwa Serikali ya China imefanya uamuzi wa kuikarabati
Reli ya Uhuru ya TAZARA inayounganisha Tanzania na Zambia na yenye urefu wa kilomita
1,860 na kusaidia uendeshaji wa reli hiyo. “Ili kutekeleza uamuzi huu kwa haraka,
napendekeza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya wataalam kuandaa ramani ya namna ya
kuitoa reli hiyo katika matatizo yake ya sasa.”
TAZARA
ndiyo reli ya kwanza duniani kujengwa na Jamhuri ya Watu wa China ambao
utaalamu wake sasa unasakwa na nchi nyingine nyingi duniani.
Rais
Jinping pia ametangaza kuwa Serikali yake itatoa nafasi 100 za masomo ya elimu
ya juu kwa wanafunzi kutoka Tanzania katika miaka mitano ijayo, itaongeza idadi
ya madaktari ambao China inapeleka Tanzania, itahimiza makampuni zaidi ya China
kuwekeza katika Uchumi wa Tanzania na kuzishawishi taasisi za kifedha za China
kuanzisha shughuli zake katika Tanzania.
Kiongozi
huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi yake itajenga chuo kikubwa cha mafunzo
ya ufundi katika Tanzania na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika eneo la
uimarishaji wa ulinzi na usalama.
Rais
Jinping amesema kuwa urafiki na uhusiano kati ya China na Tanzania ni mfano
unaong’ara wa uhusiano mzuri na mwema duniani na kuwa China iko tayari kutoa
uzoefu wake wa maendeleo kwa Tanzania bila wasiwasi wowote.
Rais
Kikwete amemshukuru sana Rais Jinping na Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada
yake ambayo baadhi yake haikutarajiwa
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
24 Oktoba, 2014.
Thank you china let see how tanzania will mange this kind of aid i hope no body is thinking of cheating.
ReplyDeleteThanks china for helping us
ReplyDeleteTanzania haihitaji kumiminiwa pesa bali inahitaji kujengewa uwezo wa kulinda rasilimali zake ikiwa ni pamoja na kuimarisha sheria za wanaokwapua pesa kaqma hizo.Mkuu wetu aombe naq msaada wa kudhibiti mchwa
ReplyDelete