Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka akisoma risala yake kwenye hafla hiyo ambapo alitoa pongezi
kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ya
Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Umoja huo kuhakikisha
malengo ya milenia yanafikiwa kwa asilimia mia moja.
Profesa Tibaijuka na Bw. Rodriguez wakijiandaa kufanya "cheers" ya kuutakia kheri Umoja huo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Tibaijuka
kuzungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez wakigonganisha glass "Cheers" kuutakia kheri Umoja huo
kwa kutimiza miaka 69.
Pichani
juu na chini baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo mabalozi na wadau wa
taasisi mbalimba za serikali na zisizoza kiserikali waliohudhuria hafla
hiyo iliyofanyika jijini Dar mwishoni mwa juma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...